Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nokia yapiga jeki mpango wa UNFPA kuhusu uzazi salama

Nokia yapiga jeki mpango wa UNFPA kuhusu uzazi salama

Kampuni ya simu ya Nokia imetangaza kuunga mkono jitihada zinazoendelea kuchukuliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na idadi ya watu UNFPA na kwa kuanzia kampuni hiyo ya simu imekubali kuchangia kiasi vifaa vya kujifungulia vipatavyo 3,000 ambayo yanakusudia kufanikisha uzazi salama.

Uchangiaji wa huduma hiyo ni sehemu ya uungwaji mkono wa kampeni iliyoanzishwa na UNFPA ambayo inahimiza uzazi salama.

Pamoja na kwamba kampeni hiyo inayotumia mitandao ya kijamii ilianzishwa rasmi mwanzoni mwa mwaka huu, lakini usambazwaji wa huduma zake unakusudia kuhakikisha kuwa watoto wanazaliwa katika mazingira salama, ikiwemo ni sehemu ya kutambua umuhimu wa kuwepo huduma za usamaria mwema. Taarifa zaidi na George Njogopa.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)