Mkutano wa IAEA kuweka mustakhbali wa matumizi ya mionzi katika tiba

4 Disemba 2012

Wataalamu wa masuala ya tiba wanaendelea na mkutano wao wa siku tano huko Bonn, Ujerumani wakiangalia jinsi mionzi inavyoweza kutumika salama katika utambuzi wa magonjwa na tiba katika muongo ujao.

Shirika la Umoja wa Mataifa la nishati ya atomiki, IAEA ambalo ndilo mwenyeji wa mkutano huo linasema kuwa takribani watu Milioni Moja hunufaika na suala la kutumia mionzi kubaini ugonjwa na kutibu kila siku.

Mathalani, wataalam hao kutoka nchi 90 na mashirika 17 ya kimataifa, wanaangalia athari za kupata kiwango kikubwa cha mionzi kupita kiasi, athari ambazo wanaweza kupata wagonjwa na wahudumu wa afya na jinsi ya kushughulikia na kuondoa athari hizo.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa IAEA Denis Flory ambaye pia ni mkuu wa idara ya usalama na ulinzi wa nyuklia kwenye shirika hilo amesema ni matarajio yao kuwa mkutano huo utawezesha kufikia makubaliano kwa manufaa ya wote kwa muongo ujao.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter