Ban azitaka serikali kuchukua hatua za dhati kuhusu ongezeko la joto duniani

4 Disemba 2012

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ametoa wito kwa serikali zilizo na uwakilishi kwenye kongamano la kimataifa la kuangazia mabadiliko ya hali ya hewa, UNFCCC mjini Doha, Qatar, kudokeza mambo matano muhimu ambayo yanaweza kukelezeka.

Bwana Ban amesema, kwanza, ameziomba ziafikie ahadi nyingine inayoandama mkataba wa Kyoto, ambao ndio ulio karibu sana na mkataba wa kimataifa kuhusu hali ya hewa.

Amezitaka pia zikubaliane kuhusu hatua za kudumu katika uwekezaji unaoambatana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Amesema pia ni lazima taasisi ziwekwe kwenye miji ya Cancun, Mexico, na Durban, Afrika Kusini ili kusaidia kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa katika nchi zinazoendelea.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

"Natarajia serikali kudhihirisha kinagaubaga kuwa mazungumzo kuhusu chombo cha kimataifa, ambacho kinaheshimika kisheraia, yapo kwenye mkondo mzuri. Serikali zinapaswa kuonyesha kuwa zina hamu ya kuchukua hatua kuhusu pengo lililopo kati ya ahadi za kukabiliana na athari za mabadiliko ya hewa na kinachotakiwa kuhakikisha joto duniani halipandi kwa zaidi ya nyuzi mbili."

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter