Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tovuti yaanzishwa ili raia wa Ghana waishio ughaibuni wachangie maendeleo ya nchi yao: IOM

Tovuti yaanzishwa ili raia wa Ghana waishio ughaibuni wachangie maendeleo ya nchi yao: IOM

Shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM, kwa kushirikiana na serikali ya Ghana imezindua tovuti yenye lengo la kuwezesha zaidi ya raia milioni Tatu wa nchi hiyo wanaoishi ughaibuni kushiriki katika maendeleo ya nchi yao.

Tovuti hiyo itakuwa ni kituo kwa waghana walio ughaibuni kuweza kupata taarifa kutoka nyumbani na hata hoja zao kuweza kushughulikiwa na serikali. Uzinduzi wa tovuti hiyo ni sehemu ya mpango wa IOM wa kushirikiana na serikali ya Ghana kuhakikisha kuna mipango tofauti ya kushirikisha ipasavyo raia wa nchi hiyo waishio ughaibuni.