Mkutano wa kutathmini mkataba wa Ottawa waanza Geneva

3 Disemba 2012

Mkutano wa mwaka wa nchi wa wanachama wa Mkataba wa kuzuia mabomu ya kutegwa ardhini yanayolengwa binadamu umeanza huko Geneva Uswisi ambapo wawakilishi wa serikali, taasisi za kiraia pamoja na wataalamu wanajadili kwa wiki nzima na kufanyia tathmini mkataba huo ujulikanao kama Ottawa Convention.

Rais wa mkutano huo Balozi Matjaz Kovacic kutoka Slovenia amesema mkutano huo umeanza wakati muafaka.

Ni siku ambayo tunatizama nyuma, miaka kumi na mitano iliyopita, disemba tatu mwaka 1997 ambapo mkataba huo ulitiwa saini na zaidi ya nchi 100 huko Ottawa, Canada. Ni siku ambayo tunakumbuka kwa nini mkataba huu unapaswa kuwepo wka sababu hii leo ni siku ya kimataifa ya siku ya watu wenye ulemavu. Na kwa bahati mbaya mabomu ya kutegwa ardhini yamewaathiri watu wenye ulemavu katika baadh iya nchi masikini zaidi duniani.”