Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wananchi wa kawaida ndio wanaondelea kutaabika zaidi nchini Syria

Wananchi wa kawaida ndio wanaondelea kutaabika zaidi nchini Syria

Wakati hali inapoendelea kuwa mbaya nchini  Syria kila siku wale wanaoiahama na waliosalia wote wanazidi kukumbwacha changamoto nyingi. Kuendelea kuwepo ukosefu wa usalama kumewapa wakati mgumu wahudumu wa kibinadamu wanaotoa misaada kwa watu walioathiriwa.

Mratibu wa masuala ya kibinadamu nchini Syria Radhouane Nouicer anasema kuwa wanajaribu kutafuta njia za kuwafikia watu zaidi wanaohitaji misaada kulingana na uwezo wao kote nchini. Hata hivyo anasema kuwa wangependa kuona ghasia zikifikia kikomo. Wito kutoka pande zote wa kutaka kuheshimiwa na kulindwa kwa maisha ya raia hakujazaa matunda na sasa watu wa kawaida ndio wanaoumia.