Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuwalinda raia ni jambo la kipaumbele wakati M23 wanaondoka Goma: OCHA

Kuwalinda raia ni jambo la kipaumbele wakati M23 wanaondoka Goma: OCHA

Siku kumi na mbili baada ya waasi wa M23 kuutwaa mji wa Goma, hali ya kibinadamu na ya kiusalama bado inatia wasiwasi katika jimbo la Kivu ya Kaskazini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Takriban watu 130, 000 wamelazimika kuhama makwao na wanaishi katika kambi na makazi mengine ya dharura karibu na, au katika mji wa Goma, wengi wao wakiwa wametoroka mapigano katika eneo hilo kwa muda wa wiki mbili zilizopita.

Katika taarifa ilotolewa leo Jumatatu, mratibu wa masuala ya kibinadamu katika DRC, Mr. Moustapha Soumare amesema kuwa wakati utekelezaji wa makubaliano ya azimio la Kampala unapoanza, na waasi wa M23 wakiondoka mji wa Goma, kuwalinda raia ni lazima kuwe jambo la kipaumbele kwa wote, kulingana na juhudi za MONUSCO na wadau wengine wa kimataifa.

Bwana Soumare amesema wakati serikali ya Kongo ikisubiriwa kurejesha udhibiti kamili wa mji wa Goma, kuna hofu ya ghasia na uporaji kutokea. Ametoa wito kwa pande zote zinazozozana kutimiza wajibu wao chini ya sheria ya kimataifa ya kibinadamu na kuwalinda raia. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(TAARIFA YA JASON NYAKUNDI)