Siku ya Ukimwi duniani

Siku ya Ukimwi duniani

Siku ya Ukimwi Duniani ni muda muafaka wa kila jamii, taifa na dunia kwa ujumla kutathmini harakati za kutokomeza ugonjwa huo ambao hadi sasa haujapatiwa tiba, zaidi ya watu kuelimishwa juu ya kinga na wale wanaoishi na virusi vya Ukimwi na Ukimwi kupatiwa dawa za kupunguza makali ya virusi hivyo.

Ripoti ya mwaka huu iliyotolewa na UNAIDS, shirika la umoja wa mataifa la kupambana na ugonjwa huo inatia matumaini kwani inaonyesha maambukizo mapya katika nchi za vipato vya chini na vya kati kama zile zilizo kusini mwa jangwa la Sahara yamepungua kwa karibu asilimia Hamsini. Na hii ni kwa sababu upatikanaji na matumizi ya dawa za kupunguza makali ya virusi hivyo umeongezeka kwa asilimia 59 na hata huduma za kupunguza maambukizi kutoka kwa mama mjamzito kwenda kwa mtoto aliye tumboni.

Mkurugenzi wa Ofisi ya UNAIDS jijini New York, Marekani. Bertil Lindblad amesema habari hizo ni njema lakini akasema unyanyapaa dhidi ya watu wenye virusi vya Ukimwi na usiri kwa watu wanaoishi na virusi hivyo ni mambo yanayopaswa kushughulikiwa. Anataka nchi kuwekeza zaidi katika mipango ya kupambana na Ukimwi badala ya kusubiri misaada.

(PKG YA GEORGE NJOGOPA)