Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pillay amtaka Rais Morsi kufikiria upya uamuzi wake wa kujiongeze madaraka

Pillay amtaka Rais Morsi kufikiria upya uamuzi wake wa kujiongeze madaraka

Kamishna wa Umoja wa Mataifa juu ya haki za Binadamu Navi Pillay amemtaka rais wa Misri Mohamed Morsi kuangalia upya tamko lililotolewa wiki iliyopita linalohalalisha kuwepo kwa katiba mpya akisema kuwa vipengele vingi kwenye tamko hilo vinakinzana na sheria za kimataifa juu ya haki za binadamu.

Kamishna huyo ameonya juu ya jaribio lolote la kupitisha katiba hiyo katika mazingira ambayo bado ni tete kunaweza kuzidisha hali ya mkwamo katika taifa hilo, lililoko kaskazini mwa Afrika.