Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Masuala ya wanawake yajadiliwe kila wakati siyo wakati wa maadhimisho tu: Eliasson

Masuala ya wanawake yajadiliwe kila wakati siyo wakati wa maadhimisho tu: Eliasson

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson amesema katika kipindi cha miaka 12 iliyopita, Baraza la Usalama la Umoja limeonyesha kuwa maamuzi yanayopitishwa na chombo hicho yanaweza kufanya maisha ya wanawake na watoto wa kike baada ya migogoro kuwa bora zaidi.

Bwana Eliasson amesema hayo katika hotuba yake hii leo wakati wa mjadala wa wazi ndani ya Baraza hilo la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu wanawake, amani na usalama.

Amesema baraza hilo limeonyesha uwezo huo kupitia maamuzi mbali mbali yanayopitishwa huku hata hivyo akisema kuwa masuala ya wanawake yanapaswa kujadiliwa wakati wote na siyo mara moja kwa mwaka.

(SAUTI YA JAN ELIASSON)