Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pillay atiwa wasi wasi na ukiukaji wa haki za binadamu kwenye maandamano nchini Tunisia

Pillay atiwa wasi wasi na ukiukaji wa haki za binadamu kwenye maandamano nchini Tunisia

Kamishina mku wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay ametoa tahadhari kutokana na ghasia zinazoendelea kwenye mji wa Siliana nchini Tunisia ambao ameishauri serikali kuhakikisha kuwa vikosi vya usalama kukoka havitumii nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji.

Maandamano hayo ya kulalamikia ukosefu wa ajira na kutokuwepo usawa kwenye maendeleo yalianza siku ya Jumanne na kusababisha makabiliano makali kati ya waandamanaji na vikosi vya usalama. Zaidi ya watu 220 wanaripotiwa kujeruhiwa siku ya Jumanne na Jumatano huku wengine wakikamatwa kutoka manyumbani mwao mjini Siliana. Kundi kutoka kwa ofisi ya mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa limewasili kwenye mji huo hii leo kutathmini hali.