Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelfu ya waliohama makwao nchini Syria bado wanaishi kwenye makao yasiyo na joto

Maelfu ya waliohama makwao nchini Syria bado wanaishi kwenye makao yasiyo na joto

Kundi la shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR nchini Syria limerejea mjini Damascus baada ya kufanya tathmini ya siku mbili mjini Homs ambapo walisema kuwa maelfu ya watu wanaliohama makwao bado wanaishi kwenye makao yasiyo na njia yoyote ya kupasha joto.

Wanasema kuwa nusu ya hospitali hazifanyi kazi na kuna uhaba mkubwa wa vifaa kuanzia madawa hadi blanketi, nguo za joto na viatu vya watoto. Akihutubia waandishi wa habari mjini Geneva msemaji wa UNHCR Melissa Fleing anasema kuwa chama mwezi mwekundu nchini Syria ambacho ni mshirika wake kimeandikisha watu 250,000 waliolazimika kuhama makwao kwenye maeneo yanayouzunguka mji huo.