Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabomu ya kutegwa ardhini yanatumiwa kwenye mpaka kati ya Syria, Lebanon na Uturuki

Mabomu ya kutegwa ardhini yanatumiwa kwenye mpaka kati ya Syria, Lebanon na Uturuki

Serikali ya Syria inaripotiwa kutumia mabomu ya kutegwa ardhini kwenye maeneo ya mpaka kati yake na Lebanon pamoja na Uturuki kwa mujibu wa Shirika la kimataifa la kupinga matumizi ya mabomu ya kutegwa ardhini. Mabomu hayo yamekuwa yakilengwa hasa kwa raia wanaojaribu kuvuka mpaka wakikimbia ghasia nchini Syria. Ripoti hiyo inasema kuwa Syria ndilo taifa ambalo limetumia mabomu kama hayo mwaka huu lakini hata hivyo makundi yaliyojihami yalitumia mabomu hayo chini Afghanistan, Colombia, Myanmar, Pakistan, Thailand na Yemen. Mark Hinzy ambaye ni mhariri wa ripoti hiyo anasema kuwa visa 4200 kutoka kwa ajali za mabomu ya kutegwa ardhini viliripotiwa mwaka 2011 ikiwa ni kama visa 12 kwa siku.

"Tuna habari kuwa kutegwa mabomu ya ardhini kunaendelea nchini Syria zikiwa ni ripoti kutoka Oktoba hadi mwaka huu. Mwezi Machi tulikuwa tumeandika kuhusu mtumizi ya mabomu ya kutegwa ardhini kwenye mpaka kati ya Syria, Uturuki na Lebanon. Kwa sasa tuna nchi moja ambayo inatumia mabomu ya kutegwa ardhini. Awali kumekuwa na nchi moja ambayo imekuwa kwenye orodha hii tangu mwaka 1999 ambayo ni Myanmar. Tumeziondoa kwenye orodha mwaka huu kutokana na ukosefu wa ushahidi kuwa serikali hizi zimekuwa zikitumia silaha hii. Kuna nchi 160 ambazo zimejiunga na mkataba wa marufuku ya mabomu ya ardhini. Nchi tatu tangu tutoe ripoti ya mwisho na hizo ni Finaland, Afrika Kusini na Somalia. Kwa kuongezwa kwa Sudan Kusini na Somalia eneo la lote la kusini mwa jangwa la sahara limejiunga na mkataba".