Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amteua Mej. Jenerali Leonard Muriuki Ngondi kuwa kamanda wa vikosi vya UM Liberia

Ban amteua Mej. Jenerali Leonard Muriuki Ngondi kuwa kamanda wa vikosi vya UM Liberia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, ametangaza leo uteuzi wa Meja Jenerali Leonard Muriuki Ngondi kutoka Kenya kama kamanda wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa Liberia, (UNMIL).

Meja Jenerali Ngondi atairithi nafasi ya Meja Jenerali Muhammad Khalid wa Pakistan, ambaye alihitimisha muda wake wa kuhudumu mnamo tarehe 9 Novemba 2012. Bwana Ban ameelezewa kufurahia mchango mkubwa wa Meja Jenerali Khalid katika kipindi cha miaka miwili ilopita, wakati muhimu ambapo uchaguzi wa kitaifa ulifanywa na kuanza harakati za kukabidhi majukumu ya UNMIL kwa serikali ya Liberia.

Meja Jenerali Ngondi ana uzoefu wa miaka 32 katika huduma ya kitaifa na kimataaifa, pamoja na uzoefu wa uongozi katika jeshi. Kabla ya kuteuliwa na Katibu Mkuu, Meja Jenerali Ngondi alikuwa kamanda wa jeshi katika mkoa wa magharibi nchini Kenya tangu mwezi Aprili mwaka 2012. Awali, alikuwa kamanda wa jeshi katika mkoa wa Mashariki tokea Novemba 2010. Amewahi kuwa naibu kamanda mkuu wa jeshi la Kenya, kati ya 2005 na 2010.