Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mbinu mpya za uwekezaji kuzingatia mabadiliko ya hali ya hewa: UNFCCC

Mbinu mpya za uwekezaji kuzingatia mabadiliko ya hali ya hewa: UNFCCC

Baraza la Kimataifa la Uchumi likishirikiana na sekritariati ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa, UNFCC, limetangaza uzinduzi wa mkakati wa “Huu ni wakati wa mabadiliko”, ambao unahusiana na uwekezaji unaojali mazingira, na ambao unaonyesha mbinu za uwekezaji katika sekta za umma na zile za kibinafsi zinazochangia kujiandaa kwa mabadiliko ya hali ya hewa na hatua za kupunguza madhara yake.

Mkakati huo ambao utazinduliwa tarehe 6 Disemba wakati wa mkutano wa Umoja wa Mataifa unaoendelea mjini Doha kuhusu Mabadiliko ya hali ya hewa, utazifahamisha serikali, wawekezaji, wafanyabiashara, mashirika ya umma ya kifedha na vyombo vya habari kuhusu njia tekelezi na mbinu za kuufanya ulimwengu ubadili tabia na kuzingatia ukuaji wa uchumi endelevu, na ambao unajali mazingira.

Akizungumza wakati wa tangazo hilo, Katibu Mkuu wa mkakati wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, Christiana Figueres, amesema ni dhahiri kuwa sekta ya kibinafsi inafaa kuwekeza zaidi katika kuuweka ulimwengu kwenye mkondo wa hali ya hewa ambayo ni salama kwa siku zijazo, huku akitaja kwamba viwango vya uwekezaji kwa sasa vipo chini zaidi ya vinvyofaa kuwa. George Njogopa na taarifa kamili

(TAARIFA YA GEORGE)