Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ajali ya moto kwenye kiwanda cha nguo Bangladesh yaishangaza ILO

Ajali ya moto kwenye kiwanda cha nguo Bangladesh yaishangaza ILO

Shirika la Kazi Duniani ILO limeelezea mshangao wake kutokana na ajali iliyotokea kwenye kiwanda kimoja cha nguo eneo la Ashulia karibu na Dhaka mji mkuu wa Bangladesh ambapo zaidi ya wafanyikazi 100 waliangamia.

ILO inatuma rambi rambi zake kwa familia za waathiriwa wa mkasa huo uliotokea mnamo tarehe 24 mwezi huu na pia kuwatakia nafuu waliojeruhiwa ambapo limesisistiza umuhimu wa kuhakikisha kuwepo mazingira salama kwa wafanyikazi maeneo ya kazi. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)