Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika ya kibinadamu kutoa misaada zaidi kwa wakimbizi Goma: OCHA

Mashirika ya kibinadamu kutoa misaada zaidi kwa wakimbizi Goma: OCHA

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA linasema kuwa mashirika ya kutoa huduma za kibinadamu yanafanya jitihada za kuwasaidia watu 140,000 kwenye sehemu 12 waliko wakimbizi wa ndani, nje na ndani mwa mji wa Goma.

Shirika la Care International limeendesha tathmini kuhusu dhuluma za kijinsia kwenye kambi za wakimbizi ambapo linatarajiwa kutoka msaada wa kisaikolojia kwa waathiriwa. Visa vya ugonjwa wa kipindupindu vimeripotiwa eneo waliko wakimbizi wa ndani kwenye kijiji cha Nzulu waliko karibu watu 5000. Jens Laerke ni msemaji wa OCHA.

(SAUTI YA JENS LEARKE)