Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

OCHA yakaribisha msaada toka Ujerumani kusaidia waathirika wa mapigano Syria

OCHA yakaribisha msaada toka Ujerumani kusaidia waathirika wa mapigano Syria

Serikali ya Ujerumani imehaidi kutoa kiasi cha Euro milioni 12 kusaidia mfuko unaoratibu majanga ya dharura kwa Syria kiasi ambacho kimetajwa kuwa ni kunakubwa kutolewa na nchi moja.

Hii ni mara ya kwanza kwa Ujerumani kuhaidi kuchangia mfuko wa majanga ya dharura unaosimamiwa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya utu wema OCHA.

Katika taarifa yake OCHA imesema kuwa kiasi hicho cha fedha kinakusudiwa kugharimia huduma za kijamii kwa mamia ya wakimbizi wa Syria ambao wakati huu wa majira ya baridi wanaandamwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ikosefu wa vifaa vya kukabiliana na baridi na huduma za madawa.