Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Fedha zahitajika kwa mipango ya kuwezesha wakimbizi wanaorejea Burundi waishi vyema: IOM

Fedha zahitajika kwa mipango ya kuwezesha wakimbizi wanaorejea Burundi waishi vyema: IOM

Shirika la uhamiaji la kimataifa, IOM linasema linahitaja dola Milioni Mbili nukta Nane kwa ajili ya kusaidia mpango wa kurejea nyumbani kwa hiari kwa wakimbizi Elfu 37 wa Burundi walioko bado nchini Tanzania.

Wakimbizi hao ni kati ya wakimbizi 39,700 wa Burundi waliokuwa wakiishi kwenye kambi mbili za Mtabila na Nyarugusu tangu vurugu za kikabila nchini mwao mwaka 1972 na 1993.

Tathmini ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR imebainika kuwa ni wakimbizi 2,700 tu kati ya hao waliobakia ndio wanahitaji hifadhi ya kimataifa na wengine warejee nyumbani.

IOM inasema kuwa wakimbizi wanaorejea makwao wanahitaji misaada ya malazi, makazi na hata mipango ya kuwawezesha waishi vizuri wakati huu ambapo tayari shirika hilo limepeleka wataalamu nchini Burundi kusaidia mamlaka za nchi hiyo kuhakikisha huduma za msingi zinapatikana kwa wakimbizi hao na jamii zinazowapokea.

Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM: