UM wataka kupunguzwa kwa gharama kwa pesa zinazotumwa nyumbani

26 Novemba 2012

Kiasi kikubwa cha pesa zinazotumwa nyumbani na wahamiaji wafanyikazi kutoka nchini maskini zaidi duniani zinatumika kusimamia gharama ya kutuma kwa mujibu wa ripoti ya shirika la biashara na maendleo la Umoja wa Mataifa UNCTAD.

Ripoti hiyo inasema kuwa gharamna ya kutuma pesa kwenda kwa mataifa ya Afrika nI mara tatu zaidi kulingana nakiwango cha wastani duniani kote.

UNCTAD inasema kuwa mifumo inayotumiwa na makampuni yanayotoa huduma za kutuma ndiyo yanafanya gharama za kutuma pesa kupanda. Mkurugenzi mkuu wa UNCTAD Supachai Panitchpakdi anasema kuwa kuna haja kwa nchi 48 maskini zaidi duniani kuboresha kuduma zao za benki na hududma zingine za kifedha ili fedha zinazotumwa kutoka mataifa ya kigeni ziweze kuwa za manufaa kwenye uchumi.