Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kufungwa uwanja wa ndege Goma kwakatiza shughuli za utoaji misaada DRC na kibinadamu: OCHA

Kufungwa uwanja wa ndege Goma kwakatiza shughuli za utoaji misaada DRC na kibinadamu: OCHA

Huku hali kwenye mji wa Goma ikibaki kuwa tete , uwanja wa ndge ambao ndio tegemeo la wafanyikazi wa kutoa huduma za kibinaadamu umebaki umefungwa na kufanya utoaji wa huduma na misaada kuwa mgumu. Mapigano makali kati ya makundi ya FARDC na M23 eneo la Masisi Magharibi mwa Goma yamesababisha kuhama kwa watu zaidi . Makadirio ya awali yanaoyesha kuwa watu 140,000 wamahama makwao ndani na nje mwa Goma watu ambao kwa sasa wanahitaji chakula na misaada mingine. Corrine Momal Vanian kutoka Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa anasema kuwa kurejesha nguvu za umeme mjini wa Goma ndicho kitu muhimu kwa kuwa ukosefu wa umeme umesababisha kutokuwepo maji safi ya kunywa.

SAUTI YA CORINNE MOMAL