Mijadala ya UM kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa sio tu kuhusu pesa, asema mtaalam wa UM

23 Novemba 2012

Mtaalam huru wa Umoja wa Mataifa, Virginia Dandan, ametoa wito kwa serikali zote duniani ziangalie gharama ya mabadiliko ya hali ya hewa kuwa zaidi ya fedha, na kuchukua msimamo wa pamoja wa kimataifa kama sehemu muhimu ya mafanikio ya mijadala ya Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, ambayo itaanza wiki ijayo mjini Doha, Qatar.

Wawakilishi kutoka nchi 194 watakutana kuanzia Novemba 26 hadi Disemba 7 mjini Doha, ili kujaribu kuongeza muda wa mkataba wa Kyoto, ambao unahusu mataifa yaloendelea kupunguza viwango vya gesi chafu angani, miongoni mwa masuala mengine. Mkataba huo wa Kyoto unatakiwa kumalizika mwishoni mwa mwaka huu.

Mtaalam huyo huru aliyeteuliwa na Baraza la Haki za Binadamu kuchunguza masuala ya muungano wa kimataifa, ameonya kuwa gharama ya ongezeko la joto duniani dhidi ya binadamu haiwezi kuepukika tu kwa kutimiza ahadi za kifedha kama njia ya kujiandaa kustahmili mabadiliko hayo. Assumpta Massoi na taarifa kamili