Ban akaribisha usitishwaji mapigano Gaza

21 Novemba 2012

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amekaribisha tangazo la kusitisha mapigano katika Gaza na kusini mwa Israel, na kuzipongeza pande zote katika mzozo huo kwa kufanya  hivyo, pamoja na Rais Morsi wa Misri kwa uongozi wake mzuri.

Akilihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ambalo limefanya kikao maalum kuhusu hali ya Mashariki ya Kati, Bwana Ban amelaani vikali mashambulizi ya kiholelaa ambayo yanaathiri raia, na kuelezea haja ya ushirikiano wa kimataifa katika kuzuia kuongezeka mapigano na kuzorota zaidi kwa hali ya usalama.

Bwana Ban amesema lililo muhimu sasa ni kuangazia juhudi zote kwenye kuhakikisha kuwa wale wote walio na mahitaji ya dharura Gaza wanapata misaada ya kibinadamu wanayohitaji. Ameongeza kuwa ni jambo la kuvuta pumzi kwa watu wa Gaza na Israel, na kwa jamii ya kimataifa kuona machafuko yanasitishwa, ingawa kila mmoja bado anafahamu hatari iliyopo, na kwamba ni lazima mengi zaidi yafanywe ili amani hiyo idumu kwa muda mrefu.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter