AU , FAO na Shirika la Lula waungana kuangamiza njaa barani Afrika

21 Novemba 2012

Tume ya muungano wa Afrika pamoja na Shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO kwa ushirikiano na shirika la Lula nchini Brazil wametangaza leo kuwa wataungana kusaidia kumaliza njaa na ukosefu wa lishe barani Afrika. Uamuzi huo ulafikiwa kwenye mkutano kati ya mweyekiti wa tume ya muugano wa Afrika Nkosazana Dlamini Zuma, Mkurugenzi mkuu wa FAO José Graziano da Silva pamoja na rais wa zamani wa Brazil Luiz Inácio Lula da Silva.

Wakati wa mkutano huo kwenye makao makuu ya muungano wa Afrika mjini Addis Ababa Ethiopia watatu hao walikubalia kuwa wataandaa mkutano utakaowajumuisha viongozi wa kimataifa na wale wa Afrika kujadili njia mpya za kumaliza njaa barani Afrika. Usalama wa chakula ni moja ya ajenda kuu ya muungano wa Afrika.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter