Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bado inawezekana kuzuia viwango vya joto duniani kupanda kwa zaidi ya nyuzi 2: UNEP

Bado inawezekana kuzuia viwango vya joto duniani kupanda kwa zaidi ya nyuzi 2: UNEP

Juhudi zaidi zinahitajika kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa bila kuchelewa ikiwa ulimwengu bado unataka kuwa na nafasi ya kuzuia viwango wastani vya joto kupanda kwa zaidi ya nyzui 2 katika karne hii.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Mpango wa Mazingira katika Umoja wa Mataifa, UNEP na Wakfu wa Hali ya Hewa ya Ulaya, viwango vya gesi chafu angani vimepanda kwa asilimia 14 zaidi ya pale vinapopaswa kuwa mwaka wa 2020.

Ripoti hiyo ambayo imetolewa siku chache kabla ya mkutano kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa mjini Doha, Qatar, inasema badala ya kupungua, gesi zinazochangia ongezeko la joto duniani kama vile carbon dioxide vimeongezeka angani kwa hadi asilimia 20 tangu mwaka 2000.