Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama la UM lapatiwa taarifa kuhusu hali ya usalama na maendeleo huko DRC

Baraza la Usalama la UM lapatiwa taarifa kuhusu hali ya usalama na maendeleo huko DRC

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limepokea ripoti ya hali ya usalama na mustakhbali wa amani na maendeleo ya kudumu katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC, ripoti iliyowasilishwa na Mkuu wa kikosi cha umoja wa Mataifa cha kulinda amani na kuweka utulivu nchini humo, Roger Meece.

Akiwasilisha ripoti hiyo ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Meece amesema harakati za kuleta amani zinaendelea huko DRC huku akisema kuwa hali ya usalama inatishiwa na vikosi vya waasi kama kile cha M23 ambacho kimeingia GOMA.

(SAUTI YA ROGER MEECE)

Mashauriano hayo ya Baraza la Usalama yamefanyika leo baada ya jana usiku baraza la usalama kupitisha azimio lenye vipengele kadha dhidi ya kitendo cha waasi wa M23 kuingia na kusonga ndani ya mji wa Goma ulioko Mashariki mwa DRC.

Azimio hilo ambalo lilipitishwa kwa kauli moja na wajumbe wote 15 wa Baraza hilo baada ya rasimu yake kuandaliwa na Ufaransa, pamoja na mambo mengine linataka waasi hao waondoke mara moja ndani ya mji huo na kupendekeza pia vikwazo.

Balozi wa Ufaransa kwenye Umoja wa Mataifa Gerard Araud alifafanua zaidi kwa waandishi wa habari kuhus yaliyomo kwenye azimio hilo.

(SAUTI YA GERARD ARAUD)