Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamishna mkuu wa UNRWA azuru Gaza kujioenea hali ilivyo

Kamishna mkuu wa UNRWA azuru Gaza kujioenea hali ilivyo

Kamishina mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina UNRWA Filipo Grandi ametembelea Gaza kujionea mwenyewe uharibifu uliofanywa na pia kukagua huduma za wafanyikzi wa UNRWA.

Bwana Grandi amekutana na wakimbizi na kuzungumza na wafanyikazi kwenye kituo cha Jabalia ambapo alielezea kuridhika kwake na kazi inayoendelea. Bwana Grandi alisisitiza kuwa hatua inayostahili kwa sasa ni usitishwaji wa mapigano. Kwa muda aa miaka minne wenyeji wa Gaza wameishi chini ya vizuizi hali ambayo imechangia kuzorota kwa uchumi wa sehemu hiyo.

(SAUTI YA FILIPO GRANDI)

UNRWA imeenddelea na operesheni  yake wakati wote wa mgogoro huu kama ilivyofaendelea na operesheni yake kwa miaka 64 iliyopita. Kwa bahati mbaya hatuwezi kusuluhisha huu mgogoro sisi wenyewe kwa kuwa UNRWA  siyo chombo cha kisiasa.Hata hivyo kazi yetu inaendelea, lakini kwa bahati mbaya shule zetu zimefungwa kwa sababu kuna hatari sana.