Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maambukizi mapya ya Ukimwi yapungua kwa zaidi ya asilimia 50 kwenye nchi 25: UNAIDS

Maambukizi mapya ya Ukimwi yapungua kwa zaidi ya asilimia 50 kwenye nchi 25: UNAIDS

Ripoti mpya ya mpango wa Umoja wa Mataifa wa kupambana na Ukimwi, UNAIDS imeonyesha kupungua kwa zaidi ya asilimia 50 ya maambukizo mapya ya virusi vya Ukimwi katika nchi 25 duniani hususan zile zilizokuwa zikiongoza kwa maambukizi mapya.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo mafanikio hayo yanatokana na kuimarishwa kwa hatua za kinga dhidi ya maambukizi ya virusi hivyo kwenye nchi za Afrika zilizo Kusini mwa jangwa la Sahara, pamoja na kupungua kwa idadi ya vifo kutokana na matumizi ya dawa za kupunguza makali ya Ukimwi.

Baadhi ya nchi zilizokuwa na idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi na ambazo kwa sasa viwango vimepungua kwa kiasi kikubwa tangu mwaka 2001 ni Malawi kwa asilimia 71, Botswana asilimia 68, Namibia asilimia 58, Zambia asilimia 50, Zimbabwe asilimia 41, Afrika kusini na Swaziland asilimia 41.

Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS Michel Sidibé amesema kasi hyo ya kupunguza kiwango cha maambukizi ni kubwa na kile ambacho kilikuwa kinachukua muongo mzima kufanikiwa sasa kinachukua miezi 24.

(SAUTI YA MICHEL SIDIBE)