Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wa UM wataka haki za watoto kulindwa

Wataalamu wa UM wataka haki za watoto kulindwa

Wataalamu watano wa ngazi za juu katika masuala ya haki za watoto kwenye Umoja wa Mataifa wamezishauri serikali kuchukua hatua zaidi za kulinda haki za watoto kutokana na dhuluma za kila aina, kuzuia ukiukaji wa haki dhidi ya watoto na kuwafikisha mbele ya sheria wale wanao wadhulumu kimapenzi watoto na kuwatumia kwemye mizozo.

Kwenye maadhimisho ya siku ya watoto duniani siku inayoadhimishwa kila tarehe ishirini mwezi Novemba, wataalamu wa Umoja wa Mataifa wameelezea sababi kuu za kutekelezwa kwa haraka mkataba wa haki za watoto na sehemu zake tatu. Wanasema sehem,u hizo zitakuwa muhimu katika kulinda watoto wakati wa amani na wakati wa mizozo pia. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)