Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Leo ni siku ya choo duniani

Leo ni siku ya choo duniani

Huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya choo duniani mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya kuwa na maji ya kunywa na usafi wa mazingira Catarina de Albuquerque amesema kuwa huenda suala la usafi lisiafikiwe kuambatana na lango la maendeleo ya milenia la kupunguza umaskini ifikapo mwaka 2015.

Mjumbe huyo amesema kuwa suala la usafi ni moja ya yale yaliyoachwa nyuma na ambalo halitaafikiwa ifikapo mwaka 2015. Anasema kuwa wale wasia na usafi wa mazingira ni watu wanaoishi kwenye umaskini makundi yaliyotengwa. Taarifa kamili na Alice Kariuki.

(SAUTI YA ALICE KARIUKI)