Kituo kipya cha runinga chatoa mafunzo kwa wanafunzi ukanda wa Gaza

19 Novemba 2012

Huku ghasia zikizidi kuchacha kwenye ukanda wa Gaza Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina UNRWA liwekuwa likitumia mfumo wake wa mawasiliano ya runinga kwa njia ya satellite kuwapa mafunzo karibu watoto 250,000 katika eneo hilo.

Runinga hiyo ijulikanayo kama UNRWA TV ni ya kwanza na ya aina yake ya Umoja wa Mataifa katika eneo la mashariki ya kati na iliundwa na wafanyikazi wa UNRWA ambao wamefanya jitihada pia za uundaji wa vipindi na kuwapa mafunzo wafanyikazi.

Huku zaidi ya shule ya shule 200 za Shirika la UNRWA zikiwa zimefungwana na kuwalazimu zaidi ya wanafunzi 200,000 kubaki nyumbani runinga ya UNRWA TV imekuwa ikitoa mafunzo wa lugha ya kiarabu, kiingereza na hesabu tangu kuanza ka mapigano. Jason Nyakundi na maelezo zaidi.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter