Hatupokei fedha kutoka kampuni za vinywaji na vyakula kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza: Dkt. Chan

19 Novemba 2012

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la afya duniani, WHO Dkt. Margaret Chan amesema kamwe shirika lake halipokei fedha zozote kutoka kampuni za kutengeneza vyakula na vinywaji ili kusaidia kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama vile saratani na moyo.

Dkt. Chan amesema licha ya kwamba magonjwa hayo husababisha asilimia 63 ya vifo vyote vinavyotokea kwa mwaka duniani kote, shirika lake limejiwekea sera madhubuti kuhakikisha kuwa kampuni hizo haziingilii mikakati ya kupambana na magonjwa hayo.

Hata hivyo ameshukuru jitihada za serikali, mashirika ya kiraia na washirika wengine ambao hufanya kazi pamoja kupunguza vifo, magonjwa na ulemavu utokanao na magonjwa hayo yasiyo ya kuambukiza. Taarifa zaidi na George Njogopa.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)