Ajenda ya maendeleo na mazingira zinategemeana: Mshauri wa Umoja wa Mataifa

16 Novemba 2012

Lengo la kutokomeza umaskini halitofikiwa bila kufanya mazingira kuwa jambo la kipaumbele, kwa mujibu wa Mshauri Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Malengo ya Maendeleo baada ya mwaka 2015, Bi. Amina J Mohammed.

Bi Mohammed amesema hayo wakati wa ziara yake kwenye ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Nairobi, ambako amehutubia maafisa wa Shirika la Mpango wa Mazingira, UNEP na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na makazi, UN Habitat, pamoja na maafisa wa ubalozi nchini Kenya. Mshauri huyo wa Katibu Mkuu amesema pia kuwa vijana ni sehemu muhimu ya agenda ya maendeleo, na kusisitiza uhusiano wa kutegemeana kati ya ajenda ya maendeleo na ajenda ya mazingira.

Katika mahojiano na Irene Mwakesi kutoka kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa, Bi Mohammed amesema vijana ni nguzo muhimu katika ajenda ya maendeleo, kwani ni wao watakaoendeleza ajenda ya siku zijazo.

(SAUTI YA AMINA MOHAMMED)