IOM yasaidia kukabiliana na Kipindupindu Haiti

16 Novemba 2012

Shirika la uhamiaji la kimataifa, IOM limechukua hatua kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu huko Haiti ulioibuka baada ya kimbunga Sandy.

IOM imesema tayari imetoa takribani vitita Elfu Kumi vyenye tembe na vifaa vingine vya tiba ya ugonjwa huo ambavyo vimesambazwa wiki hii katika kambi 31 kwenye eneo la mijini na mikoa mingine huko Haiti.

Takwimu za wizara ya afya nchini Haiti imesema hadi sasa zaidi ya watu 3,500 wamethibitika kuwa na ugonjwa huo wa kipindupindu huku watu wengine 837 wakishukiwa kuwa na ugonjwa huo kwenye mji mkuu Port au Prince na mkoa wa Upper Artibonite na wagonjwa wanatarajiwa kuongezeka. Jumbe Omari Jumbe msemaji wa IOM

(SAUTI YA JUMBE OMAR JUMBE)