Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Navi Pillay asikitika Pakistan kutekeleza hukumu ya kifo

Navi Pillay asikitika Pakistan kutekeleza hukumu ya kifo

Kamshna Mkuu wa haki za binadamu Navi Pillay ameelezea masikitiko yake juu ya taarifa kuwa Pakistani imetekeleza kwa mara ya kwanza adhabu ya kunyonga hadi kifokatika hukumu iliyotolewa miaka minne iliyopita.

Hukumu hiyo iliyotolewa mwaka 2008 na mahakama ya kijeshi dhidi ya askari mmoja ambaye alidaiwa kumua bossi wake.

Taasisi za kimataifa ikiwemo kamishana ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa ilipinga vikali hukumu kwani kwa kufanya hivyo kungekaribisha adhabu nyingine kama hizo nchini humo.

Wakati alipotembelea taifa hilo mwezi March mwaka huu Navi Pillay aliitolea mwito serikali kuondosha adhabu ya kifo na akataka pia kubadilishwa pia kwa adhabu ya kifo kwa wafungwa wengine walioko gerezani.