Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujerumani yaipiga jeki IOM kusaidia waathirika wa mafuriko Chad

Ujerumani yaipiga jeki IOM kusaidia waathirika wa mafuriko Chad

Serikali ya Ujerumani imetoa kiasi cha euro 500,000 ili kulipiga jeki shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM ambalo limechukua jukumu la kuzisaidia zaidi ya familia 38,000 zilizoathiriwa na mafuriko huko Kusin na Magharibi mwa Chad.

Mafariko hayo ambayo ni mabaya kulikumba taifa hilo yamesababisha vifo vya watu 20 na kuharibu nyumba zinazokadiriwa kufikia 94,000.

Maafisa shirika la Umoja wa Mataifa wanaohusika na misaada ya kiutu OCHA wanakadiria kuwa kiasi cya watu 700,000 wameathiriwa na mafuriko hayo ambayo pia yameharibu zaidi ya hekta za 255,720 za mazao

Kiasi hicho cha fedha kilichotolewa na serikali ya Ujerumani kitasaidia kuimarisha huduma za msingi ikiwemo chakula, makazi ya muda na huduma za kitabibu