Viwango vya UM vya haki za binadamu viwe msingi wa azimio la haki za binadamu la ASEAN

16 Novemba 2012

Jopo kubwa zaidi la wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa hii leo limetaka umoja wa nchi za kusini-mashariki mwa Asia, ASEAN kuhakikisha kuwa azimio la haki za binadamu kwa eneo hilo linalotarajiwa kuridhiwa na nchi hizo kwenye kikao chao cha Jumapili huko Cambodia, linazingatia viwango vya kimataifa vya haki za binadamu.

Michael Forst ambaye ni Mkuu wa kamati ya uratibu ya jopo hilo amesema ni vyema azimio hilo la aina yake likazingatia angalau viwango vya haki za binadamu vya kimataifa kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Jopo hilo liliundwa na Baraza la Haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kushughulikia mazingira ya kipekee ya nchi pamoja na masuala ya kimkatadha duniani kote.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud