Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yazinda kituo cha radio ya kijamii Kenya kusaidia utengamano kati ya wenyeji na wakimbizi

IOM yazinda kituo cha radio ya kijamii Kenya kusaidia utengamano kati ya wenyeji na wakimbizi

Shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM leo linazindua kituo cha radio ya kijamii kwenye mji wa Kakuma, kaskazini-Magharibi mwa Kenya kwa lengo la kusaidia kuwepo utengamano miongoni mwa wakimbizi waliko kwenye kambi ya Kakuma na wenyeji wa kabila la kiturkana wanaoishi eneo hilo.

Hatua hiyo inatokana na migogoro ya mara kwa mara kati ya wakimbizi na wenyeji hao inayotokana na vitendo vya kugombea vitu mbali mbali ikiwemo chakula cha misaada kinachosambazwa na mashirika ya misaada ya kibinadamu na rasilimali kama vile maji na malisho kwa ajili ya mifugo. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM

(SAUTI YA JUMBE OMAR JUMBE)