Nchi za Afrika zapatiwa mbinu mbadala ya kuepusha migogoro ya matumizi ya pamoja ya maji

16 Novemba 2012

Migogoro baina ya nchi za Afrika juu ya matumizi ya pamoja ya maji inaweza kupatiwa muarobaini kwa kutumia mkataba wa uhifadhi na matumizi ya pamoja ya maji ya Tume ya Umoja wa mataifa kwa masuala ya uchumi ya Ulaya, UNECE uliotumika kwa miaka 20 sasa.

Mkataba huo ulijadiliwa katika kongamano la pili la Afrika kuhusu miradi ya maji na mazingira iliyomalizika jana kwenye kituo cha Umoja wa Mataifa huko Addis Ababa, Ethiopia ili kuona jinsi ya kumaliza migogoro ya matumizi ya pamoja ya maji katika mito na maziwa barani humo na wakati huo huo kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Kongamano hilo liliandaliwa na mradi wa mazingira ulio chini ya shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP na tume ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya uchumi kwa Afrika, UNECA.

Taarifa zaidi na George Njogopa: