Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Iran ifanye uchunguzi huru wa kifo cha bloga aliyekuwa kizuizi: UM

Iran ifanye uchunguzi huru wa kifo cha bloga aliyekuwa kizuizi: UM

Jopo la wataalamu wa Umoja wa Mataifa limetaka Iran kufanya uchunguzi huru na wa kina usioegemea upande wowote kuhusu kifo cha bloga mashuhuri Sattar Behesthi kilichotokea akiwa kizuizini na uchunguzi huo uangalie madai ya kuwepo kwa utesaji na ripoti iwekwe hadharani.

Mmoja wa wataalamu hao huru wanaochunguza haki za binadamu, uhuru wa kujieleza na utesaji na mauaji nchini Iran, Ahmed Shaheed amesema licha ya kupongeza hatua ya bunge na Mahakama nchini Iran kuchunguza kifo cha Behesthi, wamesema kumekuwepo na visa vingi vya watuhumiwa kufia rumande kutokana na kuteswa, kupuuzwa na kutopatiwa tiba.

Naye Christof Heyns amesema pindi mtu anapokufa kutokana ma majeraha aliyopata akiwa rumande, kuna imani kuwa serikali inawajibika.