ILO yataja mataifa matano kwenye orodha ya mataifa 32 yanayokiuka haki ya kuhusiana

15 Novemba 2012

Shirika la kazi duniani ILO limeyataja mataifa ya Argentina, Cambodia, Ethiopia, Fiji na Peru kama mataifa yanayokiuka zaidi haki ya kuhusiana kwenye orodha ya nchi 32 zinazotajwa kuwa zinazokiuka haki ya watu kuhusiana. Kamati ya ILO inayohusika na masusla ya haki ya kuhusiana ilichunguza masuala yanayohusu haki za waajiri na vyama vya wafanyikazi za kupanga shughuli zinazowahusu.

Usimamizi wa ILO ulishughulikia mauaji ya wafanyikazi wanne na kujeruhiwa kwa wengine wawili nchini Argentina. Mauaji hayo yalifanyika wakati wa kutimuliwa kwa wafanyikazi 500 waliokuwa wakiitisha makao ya kisasa kutoka sehemu moja la ujenzi katika eneo la Mar del Plata mwaka 2009. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud