Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa Burundi nchini Tanzania waendelea kurejea nyumbani: UNHCR

Wakimbizi wa Burundi nchini Tanzania waendelea kurejea nyumbani: UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema zoezi la kurejesha makwao wakimbizi wa Burundi walioko kwenye kambi ya Mtabila nchini Tanzania linatia moyo ambapo wakimbizi wanajitokeza kwa hiari kutii agizo la serikali ya Tanzania la kuwataka warejee makwao kwa kuwa inakusudia kufunga kambi hiyo mwishoni mwa mwaka huu baada ya amani kurejea nchini Burundi.

Mwakilishi mkazi wa UNHCR nchini Tanzania CHANSA KAPAYA ametolea mfano wakimbizi wa kambi ya MTABILA iliyoko magharibi mwa Tanzania ambapo amesema takribani wakimbizi 100 hurejea nyumbani kila siku na kwamba idadi hiyo inaweza kuongezeka siku za usoni. George Njogopa na taarifa kamili:

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)