Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viwango vilivyowekwa kupunguza gesi chafuzi havijafikiwa: UNEP

Viwango vilivyowekwa kupunguza gesi chafuzi havijafikiwa: UNEP

Katika hatua nyingine, UNEP wiki ijayo itatoa ripoti yake mpya zaidi juu tofauti ya viwango vya utoaji wa gesi chafuzi duniani, ikiwa ni siku chache kabla ya kuanza kwa mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabia nchi huko Doha, Qatar.

Ripoti hiyo inaweka bayana kuwa viwango vya utoaji gesi chafuzi zinazoharibu tabaka la Ozoni ni kikubwa kuliko ilivyotarajiwa ambapo serikali zimeshindwa kutimiza wajibu wao wa kuhakikisha kiwango cha ongezeko la joto duniani hakizidi nyuzi joto Mbili kwa kipimo cha selsiyasi ifikapo mwaka 2020.

Wanasayansi 55 kutoka mataifa 22 waliandaa ripoti hiyo ambayo inapendekeza hatua kadhaa ili kufikia lengo hilo ikiwemo udhibiti katika sekta kadhaa kuanzia usafirishaji, ujenzi na misitu.