Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waasi Mashariki mwa DRC waripotiwa kuua raia wakiwemo watoto: UM

Waasi Mashariki mwa DRC waripotiwa kuua raia wakiwemo watoto: UM

Takribani raia 264 wakiwemo watoto 83 wameuawa na vikundi vya waasi wenye silaha huko Mashariki wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC, kati ya mwezi Aprili na Septemba mwaka huu.

Taarifa hizo ni kwa mujibu wa Ofisi ya Tume ya Haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa ambayo iliendesha uchunguzi wake na kubaini kuwa kikundi cha waasi kiitwacho Raia Mutomboki kilihusika zaidi na mauaji hayo yaliyochochewa mara nyingi na ghasia kubwa.

Ofisi hiyo imesema idadi kubwa ya waliouwa ni watu walioshindwa kukimbia mashambulizi ambapo wengi wao ni watoto na wazee huku takribani wanawake 12 wakiripotiwa kubakwa.

Kamishna Mkuu wa Tume ya Haki ya Binadamu ya Umoja wa Mataifa, Navi Pillay amekaririwa akiitaka serikali ya DRC kuchukua hatua za haraka kulinda raia na kukabiliana na vitendo vya ukwepaji sheria ambavyo amesema vinawalinda wauaji.

Cecile Poully ni msemaji wa ofisi ya tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa:

(SAUTI YA CECILE POULLY)