Itifaki ya kudhibiti biashara haramu ya bidhaa za tumbaku yapitishwa huko Seoul: WHO

13 Novemba 2012

Kumekuwa na hali ya matumaini juu ya mpango wa kukabiliana na wimbi la matumizi ya bidhaa zitokanazo na tumbaku na biashara haramu ya bidhaa za zao hilo ambapo mataifa wanachama wa shirika la afya duniani yanayokutana huko Seoul Korea Kusini yameridhia itifaki ya kupinga biashara hiyo.

Dkt. Haik Nikogosian ambaye anaongoza kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachoshughulikia afya na uanzishwaji wa itifaki ya kudhibiti matumizi ya bidhaa za tumbaku amesema kuwa ili ulimwengu ushinde kukabili tatizo hilo hakuna budi kuwepo kwa utashi wa pande zote,serikali na wananchi wake.

Amesema hadi sasa kuna sura ya kutia matumaini kutokana na mataifa wanachama wa WHO kuridhia itifaki hiyo ambayo imejadiliwa kwenye mkutano wa tano unaofanyika huko Seoul, Korea ukiwakutanisha wajumbe kutoka shirika la afya ulimwenguni na waitifaki wengine.

Kulingana na takwimu za WHO utumiaji wa tumbaku unachangia vifo vya watu milioni 5 wanaofariki dunia duniani kote, kiasi ambacho ni sawa na kusema kuwa mtu mmoja hufariki duniani kila baada ya sekunde sita