Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM watoa ombi la msaada kufadhili huduma za kibinadamu nchini Haiti

UM watoa ombi la msaada kufadhili huduma za kibinadamu nchini Haiti

Shirika la Kuhudumia Watoto katika Umoja wa Mataifa, UNICEF, limesema kuwa athari za kimbunga Sandy kwenye taifa la Haiti zilikuwa juu zaidi ya ilivyotarajiwa. Shirika hilo limesema mwitikio wa dharura wa sekta mbalimbali unahitajika, ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu, na kuepukana na janga la njaa na utapia mlo, ambavyo kwa jumla ni hatari zaidi hususan kwa watoto.

Ofisi ya kuratibu masuala ya misaada ya kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, OCHA, imetoa wito wa ombi la dola milioni 40 ili kukabiliana na mahitaji yanayoongezeka kutokana na athari za kimbunga Sandy.

Kwa mujibu wa OCHA, mvua kubwa na mafuriko vilisababisha uharibifu mkubwa kwenye ardhi ya kilimo, na kuongeza mahitaji hasa ya chakula. Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFP, limeonya kuwa zaidi ya watu milioni 1.5 na mahitaji ya dharura ya chakula, na huenda wasiwe na usalama wa chakula hadi mwaka 2013. Elisabeth Byrs ni msemaji wa WFP

(SAUTI YA ELISABETH BYRS)