Wanaokimbia ghasia Myanmar wazama kwenye Ghuba ya Bengal nchini Myanmar

13 Novemba 2012

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Umoja wa Wataifa UNHCR limeelezea wasi wasi kutokana na mikasa ya hivi majuzi kwenye Ghuba ya Bengal iliyowakumba watu waliokuwa wakikikimbia ghasia nchini Myanmar.

Kwa muda wa majuma mawili yaliyopita kumekuwa na ripoti za kuzama kwa mashua mbili kwenye ghuba ya Bengal zikiwa na takriban watu 240 kutoka kwa jimbo la Rakhine nchini Myanmar. Hata kama UNHCR haijathibitisha ripoti kutokana na ukosefu wa wafanyikazi wake katika eneo hilo, inasema kuwa habari inazopokea zinazsema kuwa zaidi ya watu 40 wameokolewa kutoka kwenye mashua hizo huku pia ripoti zingine zikieema kuwa miili imeonekana ikielea baharini. Melissa Fleming ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA MELLISSA FLEMING)