Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushiriki wa wakulima wadogo ni muhimu ili kufanikisha vitegauchumi vya kigeni: FAO

Ushiriki wa wakulima wadogo ni muhimu ili kufanikisha vitegauchumi vya kigeni: FAO

Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO limetoa ripoti mpya inayosema kuwa mipango yoyote ya uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya kilimo katika nchi zinazoendelea inapaswa kufanywa kwa umakini bila kuwaengua wakulima wadogo.

Ripoti hiyo iliyochapishwa leo inahusu mwelekeo na athari za vitegauchumi vya kigeni vya kilimo kwa nchi zinazoendelea na inasema kuwa uwekezaji wa kimataifa unaowapa wakulima wadogo udhibiti wa ardhi yao wenyewe ndio wenye manufaa zaidi ya kiuchumi na kijamii badala ya kuwapokonya ardhi hali inayoleta migogoro. Taarifa zaidi na George Njogopa.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)