Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza Kuu la UM lakutana kuwachagua wanachama wa Baraza la Haki za Binadamu

Baraza Kuu la UM lakutana kuwachagua wanachama wa Baraza la Haki za Binadamu

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, leo linafanya kikao maalum cha kuchagua nchi 18 zitakazokuwa wanachama wapya wa Baraza la haki za Binadamu, ili kuchukuwa nafasi ya zile ambazo muda wao umemalizika. Kulingana na kanuni za Baraza Kuu, Baraza la Haki za Binadamu linatakiwa kuwa na nchi 47 wanachama, ambazo huchaguliwa moja kwa moja kwa wingi wa kura ya siri.

Uanachama unategemea uakilishi wa kila eneo la ulimwengu, ambako maeneo ya bara la Afrika na Asia Pasifiki yana wingi wa uakilishi zaidi, yakiwa wawakilishi kumi na watatu kwa kila eneo. Kenya, Ethiopia, gabon, Ivory Coast na Siera Leone ndio wagombea kutoka bara la Afrika. Argentina, Brazil, Estonia, Ujerumani, Ugiriki, Ireland, Japan, Kazakhstan, Montenegro, Pakistan, Jamhuri ya Korea, Sweden, United Arab Emirates, Marekani, na Venezuela.

Kila taifa mwanachama wa Baraza la Haki za Binadamu huhudumu kwa kipindi cha miaka mitatu, na haliwezi kuchaguliwa tena mara tu baada ya kuhudumu kwa mihula miwili mfululizo.