Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Adhari zinazowakumba wafanyakazi wa ukusanyaji damu nchini Tanzania

Adhari zinazowakumba wafanyakazi wa ukusanyaji damu nchini Tanzania

Mara kwa mara, watu wengi hujipata wakihitaji kuongezewa damu kwa dharura. Mara nyingi, wengi huwa wamepungukiwa damu mwilini kwa sababu mbali mbali, zikiwemo ajali zinazosababisha uvujaji damu, au hata wakati wanapofanyiwa upasuaji hospitalini. Lakini ili kuongezewa damu mwilini, damu anayoongezewa mtu inapaswa kuwa salama, yaani bila magonjwa ya kuambukiza, yakiwemo magonjwa hatari kama UKIMWI.

Lakini wakati wagonjwa wakienda hospitalini kuongezewa damu, mara nyingi hawajui ni hatari gani wafanyakazi wa kukusanya damu wamekumbwa nayo wakati wakikusanya damu hiyo. Ili kufahamu zaidi kuhusu ukusanyaji damu na matatizo yepi wafanyakazi wa kukusanya damu hukumbwa nayo katika mazingira ya kufanya kazi, mwandishi wetu wa Dar es Salaam, George Njogopa, ametuandalia makala hii. Ungana naye.

(PKG YA GEORGE NJOGOPA)